Na watu walioko Al-A’rāf watawaita wanaume, miongoni mwa viongozi wa makafiri waliomo motoni, wanaowajua kwa alama zao fulani zinazowatenganisha wawaambie, «Hayakuwafaa chochote mali mliokuwa mkiyakusanya ulimwenguni wala watu; pia hakikuwafaa kiburi chenu kilichowafanya nyinyi msimuamini Mwenyezi Mungu na msiikubali haki.»