Na wale walioitika mwito wa Mola wao wa kumpwekesha Yeye na kumtii, wakasimamisha Swala za faradhi kwa namna zake katika nyakati zake, na wakitaka jambo wanashauriana juu yake , na katika mali tuliyowapa wanatoa sadaka kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, na wanatekeleza haki wanazofaradhiwa kuwapatia wanaostahiki kama vile Zaka na matumizi na katika njia nyinginezo za matumizi.