na tukawaambia wao wawili,»Endeni kwa Fir’awn na watu wake waliozikanusha dalili za uola[ wetu na uungu wetu.» Basi wakawaendea na wakawalingania wamuamini Mwenyezi Mungu, wamtii na wasimshirikishe. Wakawakanusha, na kwa hivyo tukawaangamiza maangamivu makubwa.